• Home

Vijana Brand
    • Home
    • Audio
    • Singeli
    • Singeli beat
    • Sport
    • Video
  • Breaking News

    Home / Michezo / MZEE WA KUCHETUA BM APIGWA ‘STOP’SIMBA

    MZEE WA KUCHETUA BM APIGWA ‘STOP’SIMBA

    Vijana Brand November 17, 2021 Michezo


     MZEE wa kuchetua ndani ya kikosi cha Simba, Bernard Morrison amepigwa ‘stop’ kucheza faulo za akiwa kwenye mazoezi kwa wachezaji wengine ili kuepusha maumivu yasiyokuwa na lazima.

    Novemba 16 kwenye mazoezi ya Simba yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veteran, Morrison alikuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye mazoezi hayo chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco, wasaidizi Seleman Matola, Hitimana Thiery na kocha mpya wa viungo Don Daniel.

    Katika mazoezi hayo Morrison alionekana kumchezea faulo Shomari Kapombe alipokuwa akiwania mpira jambo lililofanya Kapombe kuanguka nje ya uwanja kwa nguvu huku wachezaji wengine wakimshangaa Morrison.

    Kutokana na kitendo hicho Kapombe alionekana kupoteza ile furaha ya kuendelea kukabwa na Morrison na Hitimana alipoona hilo alionekana akimwambia Morrison aache kucheza faulo kwa kuwa hazitakiwi kwenye mazoezi.

    Morrison alionekana akijibu kwa kusema kuwa alicheza mpira na wala hajacheza faulo na alimfuata Kapombe kumpa mkono ndipo Pablo alipoamua kumfanya Morrison awe upande wa Kapombe kabla ya kuendelea na mazoezi mengine.

    Kikosi cha Simba kesho kinatarajiwa kushuka Uwanja wa CCM Kirumba kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting na tayari kimeshawasili Mwanza na Morrison ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi.

    Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kupiga hesabu ya kusepa na pointi tatu muhimu.



    MZEE WA KUCHETUA BM APIGWA ‘STOP’SIMBA MZEE WA KUCHETUA BM APIGWA ‘STOP’SIMBA Reviewed by Vijana Brand on November 17, 2021 Rating: 5
    Share This
    Facebook Twitter
    Michezo

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )
    ad inner footer

    Social Counter

    • facebook count=3.5k;
      Followers
    • twitter count=1.7k;
      Followers
    • youtube count=2.8k;
      Followers
    • pinterest count=524;
      Followers
    • instagram count=849;
      Followers
    • rss count=286;
      Followers

    mula

    Popular Posts

    • AUDIO: Sheebah – Mukama Yamba | Download
      AUDIO: Sheebah – Mukama Yamba | Download
    • VIDEO | Barnaba Ft. Alikiba – Cheketua
      VIDEO | Barnaba Ft. Alikiba – Cheketua
    • AUDIO | MC LION - NIMWAGE LADHI
    • (no title)
    • AUDIO | Anjella – Sina Bahati | Download
      AUDIO | Anjella – Sina Bahati | Download

    Recent Posts

    Comments

    Live stream

    Vijana Brand app click picha kudownlod

    Vijan Brand owner

    Blog hii inamilikiwa na Abeid Nkya Mkazi wa Dar-es-salam kuanzia Tarehe 12 February 2021 na yeye ndio mwasisi wa blog hii Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia +255688087608 Au tucheki kupitia Gmail yetu Mwadilifublog@gmail.com Vijana Brand Mziki Ni Burudani

    Recent Posts

    Recent in Sports

    Design By Vijana Brand
    Created By SoraTemplates | Distributed By Gooyaabi Templates